Ramani ya Tovuti
Hadithi
Mashairi
Hekima
- Wema hauna gharama, bali ubaya ni ghali sana.
- Salamu ni macheo ya kibinadamu.
- Amtengaye mwenzake, mwishowe hujitenga mwenyewe.
- Mfanye 'mwingine' kuwa ndugu.
- Utajiri wetu mkuu ni sisi kwa sisi.
- Sisi = Kila mtu, kila mahali.
Wao = Samahani, sijui mtu yeyote kwa jina hilo.
- Uzi mmoja hufuma yote.
- Mvulana mdogo hamwachi kamwe mwanamume, wala msichana mdogo mwanamke, hata wazeeke kiasi gani.
- Uhisani bora ni kutoa ilhamu.
- Usimchokoze mwingine kwa mchezo.
- Wema ni maambukizi bora zaidi tunayoweza kupitishiana.
- Watu wangefurahi kama ungewasalimu.
- Popote uendapo, jenga madaraja.
- Hakuna jambo la kuchekesha zaidi kuliko mtu mkatili anayeuza kadi za salamu.
- Wakati mwingine matunda matamu huota kutoka kwa mbegu chungu.
- Uwe nyumba yenye joto katikati ya dhoruba.
- Ufukara mkuu ni ukosefu wa upendo.
- Jisalimishe kwa upendo, katika kila pumzi na kila fikra, katika kila tendo na kila nia.
- Hakuna wito mkuu zaidi, wala tuzo yenye thamani kupita upendo.
- Gundua nuru kwa yule umpendaye.
- Fuata ndoto ya mapenzi.
- Gusa shauku ya mwingine, nawe utakuwa na rafiki milele.
- Ndoa imara, kama jahazi, huhitaji mkuku na tanga.
- Wapende wanafamilia wako kama uwapendavyo wageni.
- Upendo hukamilisha mambo yote.
- Siku moja wataacha kukushika mkono. Itakuwa mojawapo ya siku zenye huzuni zaidi maishani mwako. Lakini hawataacha kamwe kukukumbatia!
- Ugusapo mti, wagusa mizizi ya ulimwengu.
- Mti wa ubinadamu una shina moja, matawi mbalimbali, na mabilioni ya majani.
- Mbegu moja huotesha msitu.
- Unapokata miti, unakata viungo vya vizazi vijavyo.
- Jifunze wito wa mapenzi wa Baba Koto (kima Indri): Puaa, Puaa, Puaa.
- Sisi ni ndege wanaotatarika.
- Viumbe vyote hubeba upendo wa mama kwa mwanawe.
- Tufaha hujitenga na mti linapoanguka kutoka kwake, lakini bado ni sehemu yake kamili.
- Shakwe na mashua za tanga daima huelekea kule upepo utokako.
- Maua yote mwanzoni yalimea porini.
- Wakati mwingine miti hukua karibu sana hadi kuwa mti mmoja.
- Inashangaza jinsi sekunde 20 zinavyokuwa ndefu pale unapotulia kuzisikiliza.
- Usipite yungiyungi kwa pupa.
- Jizamishe katika pumzi ya ulimwengu unaokuzunguka.
Tulia.
- Kuona na kuonekana ni miongoni mwa zawadi adhimu zaidi za kubadilishana.
- Jifunze kusikiliza ukimya.
- Dhamiria kuishi umilele katika kila kitambo.
- Dumisha mwili mnyumbufu ili akili ibaki nyumbufu.
- Weka nje mitungi kuipokea mvua.
- Hekima hubeba uzito wa kujua.
- Yakupasa kuacha nafasi kidogo mwanzi upinde.
- Hakuna cha kufukuza.
Kila kitu kipo papa hapa.
- Njia bora ya kutunza siri ni kutomtwika mtu mzigo wa kuihifadhi.
- Nyamaza. Kunena si hisi.
- Jua linapozama, roho zetu huinuka.
- Mungu hunena kupitia machweo na mawio. Siku zote humkuta hapo.
- Hata kama
nafasi ni finyu
au muda ni mchache,
utafute umilele
ndani yake.
- Labda pumzi inayofuata ni jibu.
- Wakati wa kutazama bwawa.
- Wakati mwingine, kutotenda ndiko kutenda.
- Kuingia majini, mahangaiko huoshwa.
- Kuishi kikamilifu ni muunganiko wa kutenda na kuwa.
- Roho huonekana tu wakati akili na ubinafsi vimetulia.
- Fikiria ulimwengu wenye milima, lakini bila mabonde, majangwa, lakini bila bahari.
- Hakuna hukumu, bali kuwa tu.
- Unakuwa kile unachofikiri kila wakati.
- Sisi ni maji ndani ya kikombe na mmiminaji.
- Pinga kishawishi cha kutatiza mambo kupita kiasi.
- Dhambi hutuunda sawa na matendo mema.
- Vuta subira ndani kwa pumzi. Acha mvumo wake mwanana ukutulize.
- Kila tuta la mchanga limejaa mchanga. Acha kila seli ijae shukrani.
- Ukiwa na shaka, jaribu kujaribu.
- Zaidi ya dhoruba hii, lipo jua la milele na anga la samawati daima.
- Ubeuzi ni gugu linalopaswa kung'olewa, kamwe lisipandwe.
- Kutoshindana tena kamwe…
Kukumbatia tu…
Ni furaha iliyoje!
- Ukikimbia kwa kasi ya kutosha, waweza kukamata chembe ya theluji inayoanguka!
- Usione vikwazo visivyokuwepo.
- Amua kuwa huru.
- Thubutu si tu kuota ndoto,
bali pia kuzitimiza.
- Fanya yote uwezayo kwa yote uliyo nayo sasa hivi, sasa hivi, sasa hivi.
- Malaika anaweza kupaa, haidhuru amevunjika kiasi gani.
- Vuta ujasiri. Pumua hofu.
- Tatizo ni
kamwe huingii
kwenye pambano
bila kupigwa
wewe mwenyewe.
- Usiruhusu matukio ya kufikirika yatawale akili yako; wazia mustakabali angavu.
- Bado kuna washairi ulimwenguni.
- Kama si sasa, lini?
Katika maisha yajayo?
- Uachie ulimwengu huu kitu cha ajabu.
- Daima pendelea joie de vivre.
- Sisi ni wazazi daima wa viumbe vyetu.
- Majaribu yetu hayakomi. Bali hubadili sura.
- Usidharau kamwe umuhimu wa kumbatio.
- Tabia haijengwi kwa kuchelewa kuamka.
- Hutajutia kamwe juhudi za dhati.
- Usijifiche msituni ilhali unaweza kusimama kwenye mvua.
- Sisi ni sehemu ya wakati ujao unaotafuta kuibuka. Tukiweza kutoka nje ya nafsi zetu, wakati huo ujao unaweza kutiririka ndani yetu.
- Safari hutoa na huchukua mengi.
- Safari hutufunza kuwa tuna machache ya kuhofia.
- Utajiri wako hasa ni wema wa roho yako.
- Utajiri wako ukusanye kwa tabasamu.
- Ni jambo gani unaloliogopa zaidi, lakini unalotamani kulifanya zaidi? Hilo ni wito wako.
- Mtufaha hauzai machungwa.
- Hakuna kinachoweza kukuzuia kuwa vile ulivyo tayari.
- Safari ya ugenini ni safari ya ndani.
- Njozi zingine hukufunga. Nyingine hukupa uhuru.
- Peleka mbegu juu ya kilima. Ni jukumu lako, lakini acha mawazo yateremke chini.
- Mto daima huijua njia yake.
- Baharia hajifunzi kusafiri bila upepo.
- Kati ya nadharia na vitendo, kuna bahari.
- Wakati mwingine unahitaji kwenda milimani ili kuupata ukweli.
- Haijalishi mito ilichukua muda gani kuungana, muhimu ni kwamba hatimaye iliungana.
- Hata iwe mbali, nenda shuleni kwa miguu.
- Matendo ndiyo maneno yetu fasaha zaidi.
- Jangwani vitu vipo tu.