Kusafiri Kuelekea Orion
Safari isiyo na marejeo.
Nikisafiri kuelekea Orion
kwenye jahazi la mizimu.
Mimi, peke yangu.
Daraja la meli limetiwa giza.
Nahodha amepotea njia,
hakuna kiumbe aliyesalia,
ni safu za vyumba vitupu tu,
kamba zinazoning'inia.
Injini bado inabembeleza dhidi ya
sauti ya mawimbi yanayopiga-piga.
Mimi, peke yangu—
nimeketi kwenye omo,
kwa utulivu,
nikielekea Orion,
bila wakati,
nikisubiri kufika.
A poem by Pemba Umoja