Ungamo Kabla ya Ndoa
Harusi ya Ajabu Kuliko Zote
«Nina ungamo wa kufanya.»
«Nini?»
Anamtazama machoni pake.
«Ni nini?» anauliza.
«Ni kwamba tu. Nafikiri unapaswa kujua—kujua kabla hujaolewa nami, namaanisha.»
«Unazungumza nini? Ni nini?»
«Ni kwamba tu.»
Ni kama maneno ni makubwa mno kwa midomo yake.
«Ni kwamba tu. Mimi ni wa ajabu.»
Anamtazama, akishangaa. Mvulana huyu wa kawaida. Mvulana wake. Wa ajabu?
Akijiondolea mshangao, anajibu, «Sawa. Mimi pia ni wa ajabu.»
Safari hii yeye anamtazama, akishangaa. Msichana huyu wa kawaida. Msichana wake. Wa ajabu?
Inawezaje kuwa?
Baada ya kimya kirefu, wanabubujika kwa kicheko.
Itakuwa harusi ya ajabu kuliko zote, wanafikiri.
A story by Pemba Umoja