Karibu Nami
Maono ya huruma

Tufe la Kioo,
Ninamwona mtoto
katika ulimwengu wa kigeni.
Nitajifanya
kuwa yuko karibu nami.
Nitampa
glasi ya maji safi
na wali.
Nitampa kalamu
na kipande cha karatasi
ili ajifunze.
Tufe la Kioo,
Ninamwona mtoto
katika ulimwengu wa kigeni.
Nitajifanya
kuwa yuko karibu nami.
Shairi na Pemba Umoja