Jinsi ya Kuishi Maisha Marefu

Lulu Tatu za Hekima

Jinsi ya Kuishi Maisha Marefu — a story by Pemba Umoja

Mzee mmoja wa miaka 104 aliulizwa: “Siri yako ni nini?”

Alishiriki lulu tatu za hekima.

“Kukaa si rafiki yangu. Mwendo ni rafiki yangu.”

“Ukila sukuma wiki, mwili wako unasema asante.”

“Inapendeza kutoa salamu kwenye kioo, barabarani, na kwa maua na miti.”

Kila mtu alimcheka.

“Mzee huyu ni wa kipuuzi kweli,” walidhihaki.

Mitazamo yao na maneno yao yalimrukia kama vishale na mikuki.

Aliyadaka moja baada ya jingine na kuyarusha tena kwenye anga la buluu kwa tabasamu lenye vishimo mashavuni.

“Hiyo ndiyo siri namba nne,” alinong’ona kimoyomoyo.

Hadithi na Pemba Umoja

Misemo kutoka hadithi hii