Pengwini wa Machungwa
Hadithi Iliyotoweka
“Unafanya nini?” alisema, akimgusa Willie begani alipokuwa akiandika hadithi kwa kalamu yake.
Willie alipenda kuandika.
Alikuwa akiandika hadithi kuhusu pengwini wa machungwa.
Ndiyo, pengwini wa machungwa.
“Unafanya nini?” alisisitiza, akizidi kumgusa Willie begani.
Willie alikuwa akijaribu kuwa makini na pengwini wake wa machungwa, lakini akawapoteza machoni.
“Ninaandika. Tafadhali usinisumbue.”
Willie alijaribu kuwatafuta tena pengwini wake wa machungwa, lakini walikuwa wametoweka.
Tembo wa buluu, Willie akawaza. Nitaongeza tembo wa buluu.
Tembo wa buluu walijaribu kuwatafuta pengwini wa machungwa.
Walitafuta na kutafuta na kutafuta, lakini pengwini wa machungwa hawakuonekana.
Walikuwa wametoweka.
Kwa hiyo tembo wa buluu wakaendelea kutembea, wakijiuliza pengwini wote wa machungwa walikuwa wameenda wapi.
A story by Pemba Umoja