Yeye ni Simu ya Mkononi
Alikodolea macho simu yake ya mkononi

Tulikwenda kwenye kibanda cha kutazamia juu ya kilima.
Alikodolea macho simu yake ya mkononi.
Tulikwenda kuogelea ghubani, mji ukiwa nyuma yetu.
Alikodolea macho simu yake ya mkononi.
Tulipanda boti juu ya maji yenye mawimbi makali kando ya vilima vya kijani kibichi vya pwani.
Alikodolea macho simu yake ya mkononi.
Yeye si yeye tena.
Yeye ni simu ya mkononi.
Asubuhi anapoamka, inawaka.
Analala nayo kando yake.
Anapolala, inazimika.
Yeye na hiyo wamekuwa mmoja.
Yule yeye niliyemjua, akiomba msukumo mmoja zaidi kwenye bembea au muda kidogo zaidi katika mawimbi yanayopiga.
Yeye aliyependa kushikana mikono na alionekana kuwa na hisi ya sita.
Alijua kengele ya moto ingelia lini kabla hata haijalia.
Yeye aliyekuja akinguruma kutoka tumboni kama simba si yeye tena.
Yeye ni simu ya mkononi.
Shairi na Pemba Umoja