Mnong'ono

Kama mnong'ono angani

Mnong'ono — a poem by Pemba Umoja

Nauona mwezi
siku za jua

Kama mnong'ono angani

Uliojificha nyuma ya bahari ya samawati

Ushawahi kuota unatembea peku juu ya vumbi la mwezi?

Ukitafuta oasisi inayoakisi nyota?

Sote tunahisi joto la nyota ileile

Na kutembea kwenye mawimbi ya mwezi

Kama wazazi angani
Hawakemei kamwe
Hawatuachi kamwe.

Daima waking'aa
Daima wakimetameta

Hata nyuma ya mawingu
Hata pale
tusipoweza tena
kuwaona.

A poem by Pemba Umoja