Swali la Baba
Swali ambalo kila baba hukutana nalo.
Kaka mkubwa anamwita baba babi.
Kaka mdogo anamwita baba ba.
Kwa muda mrefu, si kaka mkubwa wala kaka mdogo alimwita baba kwa jina lolote.
Ni lini mvulana huacha kumwita baba yake babi?
Ni lini mtu mzima huanza kumwita baba yake ba?
Labda mzee au babu ndio suluhisho, ingawa yanasikika ya kizamani.
Ya kizamani mno kwa kizazi kipya.
Kwa hivyo baba huyu anapaswa kukubali babi, ba, au labda hakuna lolote.
Na bado hatujaanza kuzungumza kuhusu Mama!
A poem by Pemba Umoja