Matone ya Mvua
Matone ya mvua yakipima wakati
“Laiti ningeweza kukimbia kwenye mvua,” bibi kizee akamwambia yule kijana aliyekuwa amelowa kwa matone ya mvua.
Tikitiki ya matone ya mvua
ilianguka madirishani
ikipima wakati
kwa mawimbi madogo.
Yule kijana
alikuwa akiyaacha mawingu
akipepea na pepo za kijivu.
Yule bibi kizee
alikuwa ametua chini
akitiririka ndani ya madimbwi marefu.
Ilikuwa ni suala tu la
tikitiki.
Matone ya mvua
yakipima wakati
yakibeba hatima zetu
katika kila tone.
A poem by Pemba Umoja