Watoto wa Mshairi
kama watoto wanaosubiri kuzaliwa
Wakati mwingine mashairi hunijia
kama watoto wanaosubiri kuzaliwa
Nitapatwa na uchungu wa kujifungua
bila kalamu wala daftari machoni
nikishikilia kwa nguvu zote
kamba zao za kitovu
nikining’inia kutoka ukingoni mwa korongo
hadi nipate mahali pa kukanyaga
ukingo wa mwamba wa kupumzikia
ili niwavute watoto wangu karibu nami
ili niwaruhusu
kuja
ulimwenguni.
A poem by Pemba Umoja