Hamu ya Mzee

Safari Kwenda Baharini

Hamu ya Mzee — a story by Pemba Umoja

Kulikuwa na mzee sana. Jina lake lilikuwa Juan. Juan aliishi na mke wake, Adriana. Walikuwa wameishi pamoja kwa miaka mingi. Waliishi katika mji wenye shughuli nyingi, ndani kabisa ya bonde. Milima ilikuwa mirefu sana, vilele vyake vilizuia jua kuangaza mjini, na theluji ilianguka kwa wingi kutoka angani.

"Ninataka kuishi karibu na bahari," alisema mzee kwa mke wake, kama alivyokuwa akisema kwa zaidi ya miaka 50.

"Basi nenda ukaishi huko," alijibu yeye, kama alivyojibu kila wakati alipomuuliza kwa zaidi ya miaka 50.

Lakini wakati huu ulikuwa tofauti. Kulikuwa baridi kidogo kupita kiasi na giza kidogo kupita kiasi. Walikuwa na theluji nyingi kupita kiasi.

Wakati huu, baada ya mzee kusema, "Ninataka kuishi karibu na bahari," na baada ya mke wake kujibu kama alivyofanya kila wakati, "Basi nenda ukaishi huko," mzee kwa utulivu aliegemea fimbo yake, akajisukuma juu, akavaa koti lake, akapakia mfuko wake wa kusafiria, akafungua mlango, na bila kusema neno, akatoka nje kwenye dhoruba.

Mke wake alikuwa na shughuli nyingi na kazi zake hadi hakutambua kuwa amekwenda. Hakuinua macho yake hata kutoka kwenye karatasi zake.

Mzee alitembea akichechemea kuelekea upeo wa macho na kutoweka polepole katika safari yake kwenda baharini.

A story by Pemba Umoja