Upendo
Chini ya uso, hamu ile ile

Watu wote wale.
Wale walio kuume.
Na wale walio kushoto.
Wale walio mbele. Wale walio nyuma.
Wale walio ndani ya magari yakikimbia chini ya daraja.
Yule kijana mwenye sura ngumu.
Na yule msichana mdogo mwema.
Yule mwanaume akifungua mlango wa gari lake.
Wale wanamitindo wakitabasamu kwenye bango.
Wale wanawake watembeao haraka kwa viatu vya mchezo.
Yule mwanaume akiyumba bila viatu.
Dereva wa basi.
Yule kijana akiendesha baiskeli kwenye njia iliyojaa watu.
Watu wote wale. Wewe. Mimi. Sisi sote.
Chini ya kiburi. Ugumu. Mzaha mkali. Akili. Ubaridi. Utajiri na umaskini.
Nyuma ya jeuri. Nafsi kubwa. Kioo cha mashirika. Lugha za mitaani. Vichoro na vifungo vya shingo.
Sote tunataka.
Sote tunaota juu ya.
Sote tungekaribia kufa kwa ajili ya.
Shairi na Pemba Umoja