Machungu
Kupanda njia ya mawe

Anachowaza mwanamume wa miaka 78 anapopanda njia ya mawe yenye mwinuko mkali kuelekea nyumbani kwake mlimani:
Kulikuwa na msichana darasa la nne ambaye alikuwa hodari sana katika sanaa.
Nilikuwa nikichora pamoja naye. Alitaka kwenda shule ya sanaa. Mwishowe alikwenda.
Najiuliza nini kilimpata.
Nilipowaambia wazazi wangu kwamba nilitaka kwenda shule ya sanaa, walinikumbusha kuhusu Shangazi Kerubo. Aliota kuwa msanii na mwishowe akawa katibu muhtasi ambaye hakuolewa, katika kiwanda.
“Ukitaka kuwa msanii, kuna uwezekano mkubwa ukaishia kama Shangazi Kerubo,” walisema.
Kwa hiyo nilikwenda shule ya lugha. Angalau sasa naweza kuzungumza kwa Kiingereza.
Wazazi wangu walidhani shule ya lugha ingekuwa na manufaa zaidi.
Najiuliza maisha yangu yangekuwaje kama ningeenda shule ya sanaa.
Mwanamume huyo wa miaka 78 aliishiwa pumzi kwenye mteremko wa kilima.
Alisimama ili kutazama mandhari.
“Sasa hii ingekuwa picha nzuri ya kuchora,” alinong'ona.
Shairi na Pemba Umoja