Mtoto Mkimya
Safari Zaidi ya Milima
Alikuwepo mtoto mkimya aliyeishi katika jiji kubwa, lililozungukwa na milima.
Aliota kuhusu bahari, fukwe, machweo ya jua kwenye upeo wa bahari.
Siku moja alitoroka kupitia njia ya mlimani na akakutana na farasi wa porini aliyeitwa Claro.
Mwanzoni aliogopa.
“Je, farasi atanidhuru?” aliwaza.
Lakini basi kitu kilinong'ona ndani ya nafsi yake, naye akampanda farasi.
“Nipeleke popote upendapo,” aliamuru.
Na farasi akampeleka chini kwenye njia iliyopinda-pinda ya msituni, chini, chini, chini mlimani, kupitia bonde upande wa pili, hadi baharini.
Walisimama pamoja huku jua la rangi ya machungwa likizama chini ya bahari.
“Nimefika nyumbani,” alinong'ona kwa tabasamu.
“Nimefika nyumbani.”
A story by Pemba Umoja