Mdundo wa Tambores

Cheza, zunguka, viringika kwa mdundo wa ngoma.

Mdundo wa Tambores — a poem by Pemba Umoja

Njoo nibusu shavu, rafiki!

Mara moja nchini Uruguay.

Mara mbili nchini Argentina.

Mara tatu au zaidi ikiwa shangwe

itakushika.

Njoo cheza, zunguka, viringika katika

mbalamwezi kwa mdundo wa

Tambores.

Mdundo unadunda; uache utanue

mipaka ya roho yako—

ukutawale, ukubadili, uwe wewe.

Njoo nibusu shavu, rafiki!

Kando ya bahari ya Uruguay—

el sol, la vida,

mdundo wa Tambores.

Shairi na Pemba Umoja