Msichana Nisiyemjua Kamwe
Anakumbukwa kando ya maji

Natamani ningemjua
lakini sitamjua kamwe
Wa kwanza kupiga mbizi
ndani ya bwawa
kichwa kwanza
Wa kwanza kutembea
hadi ufukweni
lakini si kabla
ya kuwaaga
marafiki zake
kwa kucheza dansi
alizungumza
kwa mitazamo
mwendo mwororo
zaidi ya maneno
kupitia mawimbi madogo
na upepo baridi
kutoka upande mwingine
wa kumbukumbu ya samawati yenye joto
wiki zimepita
Na bado anacheza
juu ya maakisi ya maji
kwa uwazi zaidi
kuliko siku ile
nilipomwona kwa mara ya kwanza
Shairi na Pemba Umoja