Mwanga wa Nyota

Kuhusu kupenda katika ulimwengu usio na mwisho

Mwanga wa Nyota — a poem by Pemba Umoja

Napenda watu
na napenda upendo.

Moyo wangu haujai kama bakuli.
Hupanuka kama ulimwengu usio na mwisho.

Umejaa nyota
zikiangaza anga la usiku.

Labda tunachoona
ndicho tulicho.

Labda mimi ni ulimwengu.
Labda na wewe pia.

Labda mimi ni nyota katika wako.
Wewe ni moja katika wangu.

Tukiangaza sana.
Kwa mbali.

Tukitazama nyota
Mwangaza wa upendo.

Twanyoosha mikono kwa zote mbili.
Vidole vyetu vyanyooka

lakini havigusi kamwe.

A poem by Pemba Umoja