Tikisa
Wakati wino unapoisha

Kalamu yangu
inakaribia kukauka
lakini shairi langu
bado linazungumza
Mengi sana
nimeyanong'oneza tu
kwa upepo
nikitumaini
mbingu zinaweza…
tikisa,
tikisa
Kuna wino kidogo zaidi
lakini shairi
linanitoroka
mkononi mwangu
tikisa,
tikisa
tikisa
tikisa
tikisa…
Nadhani somo
ni kuwa na kalamu mbili
Shairi na Pemba Umoja