Vishinde Vidogo
Wasichana Wawili, Ubao wa Kupiga Kasia, na Maji Mazito
Walikuwa mbali katikati ya ziwa. Wasichana wawili wa miaka kumi na moja wakianza safari ya maisha.
Nitaruka hapa na kuogelea hadi ufuoni.
Njia yote?
Ndiyo, ninaweza.
Sawa, akasema yule rafiki kwa tabasamu la ujanja, huku akipiga kasia kwenda mbali, na kumwacha peke yake katikati ya ziwa.
Unakwenda mbali sana.
Unataka nije kwako?
Hapana, ninaweza. Ninajua kuogelea.
Sawa, akasema rafiki yake, akipiga kasia mbali zaidi, tabasamu lake la ujanja likipanuka.
Hee, unakwenda mbali sana.
Unataka nije nikuchukue basi?
Hapana, ninaweza. Ninajua kuogelea.
Rafiki yake alicheka kidogo.
Kuna samaki wakubwa sana huku.
Lo. Wanauma?
Ndiyo.
Inauma?
Ndiyo.
Huonekani kufika mbali sana.
Nafika. Ni kwamba wewe ndiye unayesonga.
Rafiki yake alirusha maji kwa nguvu na kasia, tabasamu lake likapanuka.
Njo unichukue. Geuka uje unichukue.
Rafiki yake aligeuza ubao wa kupiga kasia.
Mama yake na yule rafiki walicheka ufuoni.
Hee, unanicheka, Mama?
Hapana, mpenzi, tunaongea tu.
Alipanda kwenye ubao wa kupiga kasia akiwa na mashaka kidogo zaidi.
Wakienda gatini, hakuona samaki yeyote yule mkubwa.
Lazima watakuwa wameogelea mbali, mbali sana.
A story by Pemba Umoja