Harufu
Lakini harufu yao hubaki.
Nasikia harufu ya chokoleti
na moshi wa kiko
na
manukato.
Watu wengine hutembeza baiskeli.
Wengine hukaidi na kuendesha.
Jua huwaficha.
Hugeuka vivuli.
Lakini harufu yao hubaki.
Masalio ya kuwepo kwao.
Hudumu hadi upepo ujao.
Kama mdundo wa nyayo na mazungumzo
yakitoweka katika mwangwi.
Ndivyo ilivyo,
mapigo ya moyo
na pumzi zitokazo.
Vyote hivyo
vikiishiwa
na wakati.
A poem by Pemba Umoja