Mama Mpenzi
Barua iliyohifadhiwa maisha yote.
Mama Mpenzi,
Mimi nipo kwa sababu ulikuwepo, Mama.
Nakusikia ukiongea kupitia barua pekee uliyowahi kuniandikia.
Ulikuwa na mwandiko mzuri sana, Mama.
Maneno yako yalitembea kama mawimbi mchangani, sauti yako joto kama maji.
Unakuwa hai kupitia uhai wa maneno katika barua, Mama.
Maisha yako yanaanza kwenye sentensi ya kwanza.
Tena na tena na tena.
Maneno yako yanaweza kudumu milele, Mama.
Maadamu yanahuishwa.
Maneno yaliyoandikwa hutuwezesha kuongea hata baada ya kifo.
Niondokapo na maneno haya yakisomwa, tutasikiliza pamoja
bega kwa bega
na huenda tukawa hai tena
hata kama ni kwa kitambo tu.
Kwa upendo,
Pemba.
A poem by Pemba Umoja