Kubusu Ndoto
Waridi lisilofutika

Nisafiriapo duniani kote,
je, wajua
au waihisi?
Ulihisi tukibusiana
tukiruka angani?
Busu dogo
lisilosahaurika kamwe.
Kadiri nilivyojaribu
kufuta rangi ya midomo ya waridi
kutoka midomoni mwangu,
ndivyo ilivyoenea
juu mashavuni mwangu,
chini kidevuni mwangu.
Niliweza kukubeba kwa shida
tuliporuka polepole kabisa
angani,
miili yetu ikikumbatiana
katika muungano.
Sasa moyo wangu ni waridi.
Dunia yangu ni waridi.
Kila nitazamapo
ni waridi.
Shairi na Pemba Umoja