Mpanda Mlima

Hatua moja baada ya nyingine, kinyume na mantiki

Mpanda Mlima — a poem by Pemba Umoja

Nikitoka kifo

Kuingia hewa joto, ambapo mito inatiririka
Katika ndoto

Juu ya vilele vya barafu

Katika akili yako
Umeshakufa tayari
Njia elfu moja

Boti zinazama thelujini

Kama mashine
Kinyume na mantiki
Hata moyo usemapo
basi

Lakini kama pumzi
Hatua zinasonga mbele
Moja baada ya nyingine

Juu ya miguu inayotetemeka
Akili inashikilia maisha

Usiangalie juu kuona umbali gani umesalia
Usiangalie nyuma
Usiangalie chini

Hatua moja tu tena

Kisha nyingine
Na nyingine

Na…

A poem by Pemba Umoja