Kuanguka
Kujikwaa kwa Moyo

"Nilianguka kwenye barafu leo."
"Kweli? Basi je?"
"Iliniuma."
"Ndio, kawaida huuma. Watu huanguka kila wakati hapa."
"Jambo zuri nilipata bendeji."
"Ndio, ukiishi hapa, hiyo ni kawaida."
"Miezi saba ya baridi?"
"Ndio, miezi saba ya baridi. Barafu, theluji, mvua ya theluji, baridi ya kuganda."
"Oh?"
"Oh? Ikiwa hupendi, kwa nini unaishi hapa?"
"Basi, ni hadithi ndefu."
"Nina wakati."
"Kwa sababu nilianguka katika mapenzi."
"Lazima uwe umependa sana."
"Nadhani ndivyo. Nilianguka sana katika mapenzi yake wakati ule. Na tena leo. Aih."
Hadithi na Pemba Umoja